Ishu ya vyeti feki yawaondoa walimu 51 Babati

Ishu ya vyeti feki yawaondoa walimu 51 Babati



Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, inakabiliwa na upungufu wa walimu 400 wa shule za msingi, baaada ya zoezi la ukaguzi wa vyeti feki kuwaondoa kazini walimu 51, na mwisho wa mwaka huu walimu wengine 27 wakitarajia kustaafu na hivyo kutishia maendeleo ya taaluma ya elimu kwenye wilaya hiyo.

Kaimu Afisa Elimu wa wilaya ya Babati Bw Julias Sikay, ameiomba wizara ya elimu, sayansi na Teknolojia kuchukua hatua za haraka kutatua tatizo la upungufu wa walimu wa shule za msingi unaoikabili wilaya hiyo yenye shule za msingi 138 zinazomilikiwa na serikali.

Katika hatua nyingine wanafunzi 21 wameshindwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi mkoani Manyara kutokana na kupewa ujauzito, ambapo wilaya ya Babati imeelezea hatua ambazo imekuwa ikizichukua kukabiliana na changamoto hiyo.

Mkoa wa Manyara una jumla ya shule za msingi 632 na sekondari 153 zinazomilikiwa na serikali.

Post a Comment

0 Comments