Ben Pol, Barakah The Prince mambo shwari

Ben Pol, Barakah The Prince mambo shwari


Mkali wa muziki wa RnB, Ben Pol amedai uvutano wake/beef na Barakah The Prince ulishamalizika.


Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Kidume’ aliyomshirikisha Chidinma kutoka Nigeria, ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa kilichotokea ni vitu vya kawaida ambavyo vinaweza kutokea kwa kila mtu.

“Kwanza hatuna beef na Barakah, unajua sisi wote binadamu, ni wasanii wakubwa muda mwingine tunakosea kutokana na kazi zetu,” amesema.

“Muda mwingine tunakosea mbele ya kamera, mbele ya radio au mbele ya social media ikawa ni habari lakini mwisho siku hatuna tatizo tumefanya kazi pamoja, pia tumekutana mara kadhaa na kuongea kuhusu kufanya wimbo,” ameongeza.

Ben Pol na Barakah The Prince waliingia katika vita ya maneno baada ya Barakah kudai wimbo wa Ben Pol ‘Tatu’ ni mbaya.

Post a Comment

0 Comments