Bunge la Tanzania limetoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali na kusema Spika wa Bunge, Ndugai haendeshwi na serikali kama ambavyo wanasiasa wamekuwa wakisema na kudai watu hao wanalenga kumchafua, kumshambulia Spika wa Bunge na kumkosanisha na wananchi.
Katika taarifa iliyotolewa Septemba 20, 2017 na Bunge imesema kuwa kitendo cha viongozi hao kusema bunge la kumi na moja halina meno, halitekelezi wajibu wake na kudai kuwa bunge hilo na Spika wa Bunge wanaendeshwa na serikali si kweli kwani ni uongo na uzushi wenye lengo la kulichafua bunge pamoja na Spika wa Bunge Job Ndugai.
Mbali na hilo taarifa ya bunge imeweza kutolea ufafanuzi wa mambo mbalimbali ikiwepo kauli ya kusema bunge la sasa linaendeshwa kibabe, limetolewa ufafanuzi kuhusu sakata la matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu pamoja na baadhi ya viongozi kufikishwa kwenye Kamati mbalimbali za Bunge kwa ajili ya mahojiano.
0 Comments