Jinsi Kutana na kizazi kipya cha makocha vijana walivyoiteka Bundesliga

Jinsi Kutana na kizazi kipya cha makocha vijana walivyoiteka Bundesliga


Ligi kuu nchini Ujerumani Bundesliga ni kati ya ligi zenye msisimko sana, kwa jinsi soka linavyopigwa la nguvu na kukamiana.Siku za usoni kumekuwa na makocha katika ligi hiyo wenye umri mdogo sana.

Julian Nagelsmann. Kocha wa klabu ya Hoffeinheim, kwa sasa Nagelsmann ana miaka 30 na aliteuliwa kuwa kocha wa Hofeinman mwaka 2016 ina maana alikuwa na miaka 28 tu wakati huo, Julian aliichukua Hoffeinheim ikiwa na hali mbaya sana lakini msimu uliopita walimaliza katika nafasi ya 4 ya Bundesliga, wako nafasi ya 3.

Domenico Tedesco. Sio kazi rahisi sana kuwa kocha ukiwa na miaka 32 kwani katika umri huu bado watu wanapiga soka lakini Tedesco ndio kocha mkuu wa Schalke 04, kwa sasa Tadesco na timu yake wako nafasi ya 6.

Hannes Wolf(36). Stuttgart ni kati ya timu zinazowapa sana nafasi vijana na ni timu inayoamini katika msingi wa vijana, haikuwa kazi ngumu kwao kumpa kazi kocha Hannes Wolf kwa kuwa naye ni kijana mwaka 2016 akiwa na miaka 35, Stuttgart wanashika nafasi ya 12 kwa sasa.

Alexander Nouri(38). Huyu Nouri na Tadesco ni kama waliambiana wakashindane katika ukocha kwani ni marafiki wakubwa sana kabla hata hawajawa makocha, wakati Nouri anaipewa Bremen walitoka kupokea vipigo 4 mfululizo lakini alipoichukua wakacheza michezo 11 bila kupoteza mchezo hata mmoja, lakini kwa sasa Bremen wako nafasi ya 17.

Manuel Baum (38). Huyu ni mwalimu wa darasani lakini aliamua kuacha na masuala ya darasani na kuamua kwenda kufundisha academy ya soka ya Augsburg, baadaye Baum akachaguliwa kuwa kocha mkuu wa Augsburg na kuwasaidia kumaliza katika 10 la juu, wako nafasi ya 5.

Post a Comment

0 Comments