Mbunge wa Singida kaskazini na waziri wa zamani wa maliasili na utalii Lazaro Nyarandu amefika uwanja wa ndege wa Hospitali ya Hyadom kwa ajili ya dharura ya kusafirisha Mgonjwa Samson Mwaga mkazi wa Kijiji cha Mipilo Singida Kaskazini ambaye amepasuka mshipa wa kichwa.
Mbunge huyo ameandika katika Ukurasa wake wa Instagram na kusema imembidi afike kwa hara ka sana ili aweze kusaidia kusafirishwa kwa kijana huyo aweze kufika kwa haraka Hospitali ya rufaa ya KCMC Moshi.
"Nimefika hapa kwa haraka ili kumsaidia kijana huyu akapate matibabu haraka na sasa tumempandisha kwenye ndege ya shirika la Flying Medical Doctors iliyotokea Nairobi ambapo imewasili leo mchana hapa hospitalini
Ametoa shukurani kwa madaktari wote waliosimamia vyema zoezi hili hadi mgonjwa kufika Kcmc na Captain wa Ndege hiyo Mike na uongozi wake.
0 Comments