Wawili wakamatwa wakisafirisha dawa za kulevya

Wawili wakamatwa wakisafirisha dawa za kulevya


Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza linawashikilia watu wawili kwa kukutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 44 walizokuwa wakisafirisha kutoka Sirali kwenda mwanza kitendo ambacho ni kosa kisheria.

Watu hao wawili waliofahamika kwa majina ya James lawrence (51), mkazi wa Tarime – Mara, amekamatwa akiwa na mirungi kiasi cha kilo 35, aliyokuwa akisafirisha toka Sirali kwenda Mwanza kwenye bus lenye namba T.498 DAK, aina ya Youtong, na Magabe Mirumbe (45), mkazi wa Tarime –Mara, amekutwa na mirungi kiasi cha kilo 09, aliyokuwa akisafirisha kutoka Sirali kwenda Mwanza kwenye bus lenye namba T. 201 DAN aina ya Youtong, jana Septemba 22 majira ya saa mbili usiku.

Taarifa kutoka Jeshi la Polisi Mwanza inasema kuwa askari walikuwa kwenye kizuizi tajwa hapo juu wakisimamisha na kupekua magari yote yaliyokuwa yakipita kwenye barabara ya mwanza kwenda musoma, ili kuweza kubaini madereva na abiria wanaosafirisha madawa ya kulevya. aidha wakati wakiendelea kusimamisha na kupekua magari hayo waliweza kukamata magari tajwa hapo juu yakiwa na abiria hao waliokuwa wakisafirisha mirungi.

Kamanda wa polisi mkoa wa mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi amethibitisha kutkamatawa kwa watu hao na kusema kwamba anatoa wito kwa wakazi wote wa jiji na mkoa wa Mwanza na wamaeneo ya mikoa ya jirani kuacha kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya kwani ni kosa la jinai, bali wananchi wafanye kazi halali ya kujipatia kipato na wala sio vinginevyo.
Aidha pia anatoa raia kwa madereva na wamiliki wa mabasi kuacha kusafirisha madawa ya kulevya kwani kosa kisheria.

Post a Comment

0 Comments