Mambo ni hivi: Snura aeleza kinachoendelea kati yake na Shilole

Mambo ni hivi: Snura aeleza kinachoendelea kati yake na Shilole

Msanii wa muziki Bongo, Snura Mushi amefunguka kuhusu taarifa zinazodai kuwa bifu lake na Shilole bado lipo.
Muimbaji huyo amesema hakuna kitu kama hicho hata tuzo ambayo Aunt Ezekiel alitoa kwa Shilole wakati wa uzinduzi wa Filamu yake ‘Mama’ yeye ndiye alipokea.

“Sina beef hadi juzi kwa Aunt mimi sindonimempokelea zawadi, yeah, hatuna bifu na nimempelekea,” Snura ameiambia Bongo5.

Snura kwa sasa anatamba na ngoma ‘Vumbi la Mguu’ baada ya kufunika na Zungusha ambayo alimshirikisha Christian Bella.

Post a Comment

0 Comments