Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amemwambia Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kuwa wakazi wa Mkoa huo ni wachafu na wanatia aibu.
Makonda ameyasema hayo katika Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani, ambapo amesema kuwa usafi ni tatizo kubwa katika mkoa huo.
“Usafi ni moja ya tatizo kubwa katika Mkoa wa Dar es Salaam, na kwa kweli tunavyoonekana ni wastarabu na baadhi ya Mikoa mingi wanatamani kuwaona wajanja wa Dar es Salaam, lakini ukweli usiofichika Mh. Makamu wa Rais Dar es Salaam ni wachafu na wanatia aibu,” alisema RC Makonda.
0 Comments