Diamond amtumia ujumbe mzito mama yake ‘nikifa kesho nusu ya mali zangu ni zako’

Diamond amtumia ujumbe mzito mama yake ‘nikifa kesho nusu ya mali zangu ni zako’

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz leo Julai 7, 2018 amesema kuwa endapo itatokea kesho akaaga dunia basi nusu ya mali zake zitachukuliwa na mama yake mzazi.

Diamond Platnumz

Akitoa ujumbe huo wa kum-wish mama yake siku ya kuzaliwa kupitia ukurasa wake wa Instagram, Diamond amesema mama yake amepitia magumu mengi sana ikiwemo manyanyaso wakati akimlea hivyo hakuna mtu wa kumlinganisha na mama yake.

“Nasikitikaga sana Wanapojaribu Kulinganisha Thamani yako kwangu na Mtu yoyote…Na kusahau kuwa pasipo wewe kunizaa na Kunilea kwa shida na tabu leo hii hakuna yoyote ambae angeniona wamaana….. Ikiwa wewe ndio Ulonifanya mie nikawa Duniani Basi you will always be My First priority then the rest will follow…Dharau na Manyanyaso Ulopitia kwenye kunilea Hakuna anayejua, Tabu na shida Ulizopitia kufanya hadi leo walau nionekane mtu mbele za watu.. eti mtu kirahisi tu anatokea na kukuringanisha na mtu… Mama MADALE is your House!!! na ikitokea kesho nimekufa pia NUSU ya Mali zangu zote ni zako.“ameandika Diamond Platnumz.

Nakusisitiza kuwa anapambana kwa ajili yake ili kumfanya awe na furaha katika muda wake wa maisha uliosalia “Mwanao Napambana Usiku na Mchana Kwanza kwajili yako, Walau Ujifariji kwa Magumu Ulopitia kwa kunilea kwangu, i want you to Enjoy the life as Much as You can, Maana sina cha kukulipa zaidi ya Hicho..HAPPY BIRTHDAY MAMA I LOVE YOU SANA,“.

Leo Julai 7, 2018 Mama yake na Diamond Platnumz, Sandra anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.

Post a Comment

0 Comments