Klabu ya Singida United imefanikiwa kuingia kandarasi ya miaka mitatu na aliyekuwa mlindalango wa Njombe Mji FC, David Kisu.
Kisu anayetokea klabu ya Njombe Mji aliwahi pata nafasi ya kuwatumikia mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba msimu wa mwaka 2017/18 .
Usajili wa mlindalango huyo ulichelewa kutokana na mambo ya kandarasi yake na waajiri wake hao wapya kutokuwa sawa.
Mpaka sasa Singida United inafikisha jumla ya walindalango watatu ambao ni Manyika Peter Jr, Ally Mustapha na David Kisu.
0 Comments