Real Madrid imewasiliana na klabu ya Juventus ya nchini Itali ili kufanya mazungumzo ya ana kwa ana juu ya mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo.
Wakala wa Ronaldo, Jorge Mendes ameambiwa na Mkurugenzi Mkuu wa klabu ya Real Madrid, Jose Angel Sanchez kuhakikisha Juve wanatoa kiasi cha fedha euro milioni 100 sawana pauni milioni 88 ili kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33.
Mendes anaamini kuwa Juventus wanaweza kumudu gharama hizo zinazohitajika na Madrid ili kufikia muafaka wa kumuachia Ronaldo kujiunga na miamba hiyo ya Italia
0 Comments