Mkuu wa mkoa Godfrey Zambi atoa onyo kali

Mkuu wa mkoa Godfrey Zambi atoa onyo kali


Mkuu wa mkoa wa Lindi na Mwenyekiti wa ulinzi na usalama mkoa huo,Mhe.Godfrey Zambi, amesema hatasita kumchukulia hatua kali kiongozi yeyote anayediliki kutumia majukwaa kuwapotosha wananchi kwa kutoa kauli za uchochezi ambazo zinaweza kusababisha vurugu.
"Sitamwangalia kiongozi anayesababisha vurugu kwenye mkoa wangu," amesema Mhe. Zambi.
Kiongozi huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuchukizwa na kitendo cha mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Liwale, Mohamedi Mtesa kutamka maneno ya uchochezi wakati wa mkutano wake na wananchi wa wilaya hiyo.
Mhe. Zambi amesema kuwa atawafikisha mbele ya vyombo vya sheria viongozi hao wapotoshaji.

Post a Comment

0 Comments