Steve Nyerere atoa ya Moyoni kuhusu Jokate kuteuliwa

Steve Nyerere atoa ya Moyoni kuhusu Jokate kuteuliwa


Kumekuwa na picha kadhaa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimkejeli Steve Nyerere na kumkashfu kuhusiana na uteuzi uliofanywa na Rais Magufuli na kumteua Jokate Mwegelo kama Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe.

Huku wengi wakisema kuwa kutokana na Steve Nyerere kuipigania CCM lakini hajachaguliwa katika nafasi yoyote serikalini kupitia ukurasa wake wa instagram amefunguka ya moyoni kuhusiana na kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii.

“Tumekuwa watu wa kuongelea watu katika mifumo isiyo stahili. Kama vijana tunatakiwa kujivunia wenzetu waliopewa dhamana na RAIS, si kuanza kuwachafua na kuwaona hawafai tunasahau hakuna binadamu sahiii wote tuna mapungufu. Sasa basi tukianza hesabu zambi za kila mmoja nadhani si jambo jema.’


“Nia ni TANZANIA kwanza embu tuiweke akili yetu kwenye maendeleo yenye tija naamini mwendawazimu ni yule ambaye anakosa UZALENDO kwenye TAIFA lake. Tuwe WAZALENDO hata kidogo tu hii mitandao inatufanya hata wenye akili wanaonekana majuha”

Post a Comment

0 Comments