Steve Nyerere atangaza kurudi tena kusimamia misiba, "Nimeona utendaji hauniridhishi"

Steve Nyerere atangaza kurudi tena kusimamia misiba, "Nimeona utendaji hauniridhishi"



Baada ya kuonekana kujiweka pembeni katika kamati za jusimamia msiba wa marehemu Mzee Majuto, Steve Nyerere ametangaza kurudi tena.

Akiongea na kipindi cha Le3o Tena cha Clouds FM, muigizaji huyo amesema sababu kubwa iliyomfanya arudi kusimamia mambo hayo ni kutokana na kutoridhishwa na utendaji kazi wa usimamizi wa misiba unaofanywa wakati yeye amejiweka pembeni.

"Mimi sitaacha kusimamia misiba kwa sababu ya maneno ya watu. Nilikaa pembeni lakini nimeona utendaji hauniridhishi hivyo imebidi nirudi, baadhi ya watu kazi yao kuchuruza maji kama dodoki na niwaambie hakuna msiba wenye faida," amesema Steve.

Msanii huyo na amekuwa akituhumiwa kula fedha za michango ikiwemo kwenye misiba wa marehemu Agnes Masogange.

Post a Comment

0 Comments