Zaidi ya Shilingi Milioni 560 zimetengwa katika ujenzi wa zahanati

Zaidi ya Shilingi Milioni 560 zimetengwa katika ujenzi wa zahanati



Na James Timber, Mwanza

Jumla ya fedha shilingi milioni 561 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati kwenye Kata Tano zilizopo katika Jimbo la Nyamagana jijini Mwanza.

Akizungumza na Vyombo vya Habari katika Ziara yake ya kukagua ujenzi wa Zahanati katika Jimbo hilo Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula alisema kuwa lengo kubwa ni kuboresha huduma za afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuwasogezea huduma hiyo karibu tofauti na hapo awali walipokuwa wakiifuata umbali mrefu.

Mabula alibainisha kata zilizopata fedha hizo kuwa ni pamoja na Isamilo shilingi milioni 107, Bugarika shilingi milioni 67, Mahina shilingi milioni 87 na Kata za Mhandu na Mkuyuni zilizopokea kiasi cha shilingi milioni 150 kila kata.

Aidha Mbunge huyo alifafanua chanzo cha fedha hizo kuwa ni kutokana na makusanyo ya ndani ya mapato huku akimpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza James Bwire kwa kuwa kipaumbele katika kuboresha sekta ya afya katika Jiji hilo.

Post a Comment

0 Comments