Duma Akifanikiwa Mtasema Freemason

Duma Akifanikiwa Mtasema Freemason



Meneja wa msanii wa filamu bongo, Daudi Michael maarufu kama Duma, Maneno amedai kwamba hashangazwi na tuhuma za ushirikina zinazomuandama mfanyakazi wake huyo kwa kuwa hata siku akija kufanikiwa watu watamuita ni Freemason.

Meneja Maneno amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye eNewz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, baada ya kuwepo tetesi kuwa Duma alitumia uchawi katika uzinduzi wa filamu yake mpya ya 'Nipe Changu' iliyozinduliwa Mliman City jijini Dar es Salaam, na kufanikiwa kujaza watu wengi licha ya kuwa kazi yake haifanani na uwingi huo.

"Tuhuma za ushirikina zipo maana huwezi kuwakatalia watanzania kwasababu mwisho wa siku Duma akifanikiwa watasema ni Freemason na kuongea mambo mengi juu yake. Kwa hiyo kuongelewa ipo na unapokuwa maarufu kuongelewa ni jambo la kawaida", amesema Meneja Maneno.

Pamoja na hayo, Meneja Maneno ameendelea kwa kusema "tasnia ya filamu inahitaji nguvu, mashambulizi na mabadiliko 'so' ndio maana nikaamua kujikita kwa ndugu yangu Duma, ili niweze kushirikiana naye kuleta kitu ambacho kitakuwa na tija kwa watanzania. Ninaamini watu watajifunza vingi kutoka kwa Duma".

Aidha, Meneja Maneno amekiri kwamba alishawahi kwenda kwa waganga kuloga ili wasanii wake wafanye vizuri kwenye kazi zake japokuwa alikuwa hafahamu kuwa waganga nao wanamtegemea Mungu.

"Kwa mganga ni kama nyumba tu au 'gheto', unaenda unapiga stori freshi tu. Nilikuwa sijajua kwamba mganga naye ana muomba Mungu kwasababu kama kweli angekuwa na nguvu basi angesababisha watoto wake waolewe na viongozi wa nchi lakini kwasababu hana uwezo huo, wote wanasugua rumba na kunyunyiza dawa. Kwa hiyo ukimuamini Mungu utafanikiwa kwa kila jambo, mimi ninaamini Duma anachokifanya ni uwepo wa Mwenyezi Mungu pia", amesisitiza Maneno.

Post a Comment

0 Comments