Anayedaiwa kutobolewa macho na Scorpion afunguka kuachana na mkewe

Anayedaiwa kutobolewa macho na Scorpion afunguka kuachana na mkewe


Kijana Said Mrisho aliedaiwa kutobolewa macho mwaka jana maeneo ya Buguruni, Sheli jijini Dar es Salaam, amefunguka juu ya tuhuma zinazo mkabiri juu ya kuitelekeza familia yake. 


Kupitia kipindi cha Leo Tena, Clouds Fm Said Mrisho amejibu tuhuma hizo zilizotolewa na mkewe Stara Soud kuwa hajatelekeza famila yake ila amechana na mke wake huyo na sasa ameoa mke mwingine na ndoa ya mke huyu aliye naye sasa ni shinikizo kutoka kwa wazazi wa mke wa kwanza ili wakiachana wagawane mali. 

“Ni kweli nimeachana na mke wangu ambaye nimefunga nae ndoa hivi karibuni baada ya kupata matatizo, ila sijatelekeza familia, na hii ndoa nimefunga kutokana na shinikizo kutoka kwa wazazi wa mke wangu ili tukiachana tuweze kugawana vifaa vilivyokuja (mali). Japokuwa tumeachana lakini nimempangia nyumba na namsaidia kwasababu nina familia nae. Kwa sasa nimeoa mke mwingine,” ameeleza Said. 

Pia ameongeza kuwa “Mke wangu nimemuacha sababu ya tabia zake mwanzoni nikiwa naona alikuwa akinisaliti lakini hata sasa anaendelea kunisaliti, Siku moja aliniomba simu akaniambia anaomba simu ampigie mtu aliyemkopesha pesa hospitali. Nilimpatia simu mama dee na akatoka lakini alichelewa kurudi nikamuuliza vipi akasema alikuwa hapatikani lakini baadaye nikabonyeza button ya kupiga. Nilipopiga simu akapokea mwanaume mwingine nikamuuliza vipi akaniambia huyu ni mke wake kivipi wakati ni mke wangu mimi. Japokuwa nimepata zile bajaji huwezi kuamini navyonyanyasika kwenye familia yao hata hesabu za siku hawaleti. ” 

Baba Dee anaendela kusimulia “Mke wangu amenifanyia vitu vingi vya ajabu anapigiwa simu na wanaume na hao wanaume wananitukana nilimweleza baba yake akaniambia nimpe talaka au nimuoe mwanamke mwingine, amekuwa mlevi anaweza hata kumuingiza mwanaume mwingine chumbani kwangu kwa sababu sioni kwakweli nilishindwa kuvumilia hasa kutokana na hali yangu.” 

Baba Dee ameeleza kuwa watu wangi wanajua yeye ana pesa baada ya kupewa bajaji ila mpaka sasa ni miezi sita tangia ampatie kaka yake na mke wake bajaji hawajampatia mahesabu. 

Kupitia kipindi hicho hicho naye mkewe Mama Dee amekuwa sababu zinazotolewa na mumewe ni uongo na hakuna jambo lenye ukweli hata kidogo. 

“Kinachoshangaza Saidi alitafuta nyumba nyingine tena akahamisha vitu kule kwenye nyumba ya Tabata lakini mimi alinidanganya. Nilipomuuliza Makabati yako wapi akasema yapo kwa fundi nimeyapeleka kupakwa rangi kwa fundi kumbe muongo kampangisha mwanamke ambaye amemuoa mwezi wa Ramadhani,” amesimulia mke wake na Said 

Amesisitiza mke huyo “Anasema haniamini hata chakula ninachompikia anahisi nitamwekea sumu kwa sababu haoni, kwanini nisimwekee sumu wakati alipopata matatizo nimekaa naye hospitali muda mrefu nikimuuguza, nikimuogesha na kumfanyia kila kitu.”

Post a Comment

0 Comments