Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wa klabu hiyo Geofrey Nyange Kaburu wamenyimwa dhamana kwa kesi inayowakabili.
Aveva na mwenzake watarudi rumande hadi Julai 20 mwaka huu, hatua hiyo imetolewa leo na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Victoria Nongwa.
Kwa mujibu wa kesi inayowakabili viongozi hao wana mashtaka matano ambapo mawili kati ya hayo ni ya kutakatisha fedha, wamekosa dhamani kwa kesi yao ya utakatishaji fedha.
0 Comments