Beki kisiki wa timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves amejiunga na klabu ya PSG ya Ufaransa kwa mkataba wa miaka miwili.
Mchezaji huyo ambaye msimu uliopita alijiunga na Juventus ya Italia akitokea Barcelona, amesaini mkataba huo ambao utamalizika Juni 30, 2019.
Awali mchezaji huyo ambaye alikuwa huru kujiunga na timu yoyote baada ya kumalizana na Juve, alitajwa kuwa na uwezekano mkubwa wa kutua Manchester City na kuungana na kocha wake wa zamani Pep Guadiola.
Alves ameshinda Jumla ya vikombe 33 akiwa na vilabu tofauti tofauti, ikiwemo mataji matatu ya Uefa akiwa na Barca.
0 Comments