Baba wa Maundo Zoro awajia juu Shilawadu

Baba wa Maundo Zoro awajia juu Shilawadu


Baba mzazi wa mwanamuziki Maunda Zoro na Banana Zorro, mzee Zahir Zorro amewajibu wanoandika habari kuwa binti yake amekongoroka.


Kupitia mtandao wa Instagram, mzee huyo ambaye pia ni mwanamuziki amewawakia watu wanaopakaza kuwa binti yake amekongoroka kutokana na matumizi ya pombe haramu ya Gongo pamoja na madawa ya kulevya aina ya Bangi.


Aisee, huyu ndie Maunda Zorro wangu Shillawadu wanadai amekongoloka na Gongo na Bangi. Ajabu Waajiriwa wa Media ya Sifa Wanaandika bila ku- Balance Khadithi. Walienda Muhoji Hawa niliye mlea kwangu kama Binti yangu zaidi ya Miaka miwili. Akaondoka, Akarudi baadae Akaondoka tena bila kufukuzwa. Leo anajaribu kuukata Mkono uliomlisha kwa Wembe. Waniombe Radhi!

Shilawadu wanapaswa kufahamu hili, umaweza Wadanganya Watu wote muda au kipindi Fulani tu. Hutoweza kuwadanganya Watu Muda au Kipindi chote. Nawaambia kwa hili Wamechemsha!

Mama yake na msanii Hawa wa Nitarejea alinukuliwa akisema katika kipindi cha Shilawadu kuwa Maunda Zoro na binti yake ni marafiki na huwa wanavuta bangi na kunywa gongo nyumbani kwake.

Post a Comment

0 Comments