Brandy atemana na mpenzi wake mpya

Brandy atemana na mpenzi wake mpya

Mkali wa muziki wa RnB nchini Marekani, Brandy ambaye amekuwa akitoka kimapenzi na producer wa muziki Sir Baptist wanadaiwa kutemana.


Brandy na mpenzi wake ambaye walianza kuonyesha mahaba yao kupitia mtandao wa Instagram, wemetemana baada ya mrembo huyo kumfumania na kimwana kingine.

Tukio la wawili hao kutemana limekuja baada ya mzazi mwenzake na SirTheBaptist, kukiri kuwa bado wana mahusiano kitu ambacho Brandy alikuwa hakijui.

Hata hivyo haikuishia hapo chanzo cha karibu kimeeleza kuwa ““Once Brandy saw that IG live video, it was a done deal.” They added, “When she sees red flags, that means it’s time to go and that was one too many. She would rather be alone than unhappy!”

Hii imekuwa ni tabia ya mwanaume huyo kusaliti wapenzi wake, inadaiwa kuwa Sir John aliachana na mpenzi wake Shenanigans, baada ya kubambwa akimsaliti na mwanamke mwingine.

Post a Comment

0 Comments