Rapper na Msemaji wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili ameeleza kushangazwa na namna media zinahaoji kipi kifanyike ili muziki wa Bongo Flava ukue wakati huo haziruhusu wasanii kutoa hit nyingi kwa wakati mmoja.
Nikki ambaye anabamba na ngoma ‘Quality Time’ pamoja na ‘Amsha Dude’ ya Weusi, ameeleza kuwa wasanii wa nje wamekuwa wakitoa nyimbo nyingi kwa wakati mmoja na media za hapa Bongo zimekuwa zikisapoti.
Kupitia mtandao wa instagram Nikki ameandika ” Drake, Wizi Kid, Davido, Dj khalid, Major Lazer nawasikia kwenye media mbali mbali hapa nyumbani wakisifiwa kuwa wanakimbiza kwakuwa wana hits nyingi kwa wakati mmoja.
“Lakini kama msemaji wa Weusi nimekuwa nikihojiwa na media kibao kuwa kwanini mmetoa hits zenu haraka haraka hamuoni mnauwa track zenu wenyewe????? halafu hapo hapo wanakuuliza nini kifanyike ili muziki wa Tanzania ukue???? Kazi itakuwaje kama wafanyakazi wakifanya kazi wanaambiwa wanauwa kazi???,” amehoji Nikki.
0 Comments