Country Boy ana mpango wa kuwakutanisha Diamond na Alikiba

Country Boy ana mpango wa kuwakutanisha Diamond na Alikiba


Rapper kutoka kwenye Bongo Flava, Country Boy amedai kuwa moja ya mipango yake ni kuja kufanya ngoma na Diamond na Alikiba.


Country Boy amesema mpango huo ni katika kuhakikisha kuwa muziki wake unakuwa na sound ya tofauti, lakini hata hivyo kila mmoja atakuwa na ngoma yake.

“Round hii nataka nilete different sound kwa sababu tayari am rapper nataka nitengeneze sound mpya. Nawataka hawa malegendary wawili, hapa Alikiba, hapa Diamond ila siwashirikishi katika track moja, kila mtu na ngoma yake,” ameiambia Daladala Beat ya Magic Fm na kuongeza.

“Kila mtu na upande wake natengeneza sound mpya, nahisi nitaleta kitu kikubwa. Ninachoshukuru kwa Mungu mimi nipo flexible naweza kurap katika beat yoyote,” amesisitiza.

Katika hatua nyingine Country Boy amewataja wasanii wa kike anaotamani kufanya nao kazi, “kwa upande wa wadada nampenda sana Vanessa Mdee na Nandy, wanaimba vizuri sana nikisikiliza ngoma zao namsikia Mariah Carey, nasikia muziki mzuri sana,” amemaliza kwa kusema.

Post a Comment

0 Comments