Mchezo wa kirafiki wa kuhitimisha michuano ya SportPesa Super Cup baina ya Everton dhidi ya Gor Mahia umemalizika huku The blues ikichomoza na ushindi wa magoli 2 -1.
Katika mchezo huo uliokuwa na mvuto wa kipekee hasa kwa mabingwa wa SportPesa Super Cup timu ya Gor Mahia kuonekana kuumudu mchezo huo na kupelekea kutoka sare ya goli moja moja hadi dakika 45 za kipindi cha kwanza kinamalizika.
Katika kipindi hicho cha kwanza mchezaji Wayne Rooney ndiye aliyekuwa kivutio kikubwa mara baada ya kuliona lango la Gor Mahia baada ya kupiga mpira ulioenda moja kwa moja nyavuni na kujiwekea historia nyingine kwa kufunga goli lake la kwanza toka arejee katika Everton katika usajili wa msimu huu.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Bongo5 imezungumza na Mkurugenzi wa SportPesa, Abbas Tarimba na kuwashukuru wa Tanzania kujitokeza kwa wingi.
“Tunafurahi kuona watu wamejitokeza kwa wingi na kuthibitisha kuwa mpira unapendwa Tanzania”. Amesema Tarimba ambaye ni Mkurugenzi wa SportPesa.
Tarimba ameongeza kuwa “Yapo mambo ya kujifunza na tutakaachini na kuangalia namna ya kurekebisha, ila tunawashukuru wa Tanzania kwa kujitokeza kwa wingi”.
0 Comments