Linex adai ujauzito wa mpenzi wake ulimpoteza kwenye game

Linex adai ujauzito wa mpenzi wake ulimpoteza kwenye game


Msanii wa Bongo Flava, Linex amedai kuwa kutokana na kulea ujauzito wa mpenzi wake kulimfanya kutosikika katika muziki.


Muimbaji huyo ambaye ameachia ngoma mpya ‘Got Me’, ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa kitu hicho anajivunia ni mara chache sana mwanamke kupata mwanaume wa aina yake.

“Kwa mfano mimi nina mtoto sasa hivi kwa hiyo nilikuwa nalea, miezi tisa ya kucheza na mama mtu, nilijsikia tu kumjali kuanzia mwanzo. Halafu ni bahati si rahisi kupata mwanaume ambaye anamjali mwanamke kuanzia mwezi mmoja mpaka tisa,” amesema Linex.

June 27 mwaka huu Linex alitangaza kupata mtoto wa kiume na kumpatia jina la Jaheim.

Post a Comment

0 Comments