Kesi ya viongozi wa Simba yasogezwa mbele

Kesi ya viongozi wa Simba yasogezwa mbele


Kesi inayowakabili rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva na makamu wake, Godfrey Nyange ‘Kaburu’ imekhairishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo na kutarajiwa kusikilizwa tena julai 31 mwaka huu.


Aveva na Kaburu wanakabiliwa na tuhuma za kughushi nyaraka za Simba SC na kutakatisha dola 300,000 (zaidi ya Sh milioni 650) na wamekuwa mahabusu tangu Juni 29, mwaka huu.

Hii leo katika mahakama ya Hakimu Mkazi kisutu rais wa Simba, Aveva amefika mahakamani peke yake wakati wa kesi hiyo.

Kabla ya kutajwa kwa kesi hiyo wanachama wa Simba walianza kufika mahakamani mapema ili kujua hatima ya viongozi wao.

Post a Comment

0 Comments