Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger ameonekana kuzua gumzo baada ya kuonekana kuvaa raba ambazo si kawaida yake.
Raba hiyo imegeuka imekuwa gumzo baada ya kuonekana ni kiatu maalum chenye nembo ya Arsenal.
Wenger alikuwa katika bench wakati Arsenal ilipoifunga Bayern Munich kwa mabao 3-2 kupitia mikwaju ya penalti katika michuano ya ICC.
Katika benchi Wenger alikuwa na wasaidizi wake kocha wa makipa Jens Lehmann pia Vic Akers katika mchezo huo ameonekana kutokuwa na shaka na kudhihirisha kuwa yeye ni Arsenal damu mapenzi yake kwa klabu hiyo yapo ndani ya moyo.
Wenger amekuwa kocha wa muda mrefu ndani ya Arseanal ameonekana akiisifia rangi ya kiatu chake wakati akikitambulisha kwa mara ya kwanza nchini China.
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 67 ameonekana kuvalia sare za Arsenal katika michuano ya kimataifa ya kombe la mabingwa (ICC) huko Shanghai.
0 Comments