Mbunge wa Singida Mashariki, na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu akataa kuondoka chumba cha Mahakama ya Wilaya ya Dodoma jana, akidai kuwa ana taarifa ya kutakiwa kukamatwa na kupelekwa jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo lililotokea mahakamani hapo jana, hali hiyo ilitokea mara baada ya kuahirishwa kwa kesi ya Chama cha Walimu Manispaa ya Dodoma (CWT)iliyokuwa inahusu mgogoro wa viongozi wa chama hicho wanaodaiwa kufanya matumizi mabaya ya mali za chama hicho.
Lissu alisema amepata taarifa za kutaka kukamatwa kupitia ujumbe mfupi aliotumiwa na Mkewe toka Dar es salaam ambapo asubuhi askari walifika nyumbani kwake na kujulishwa kuwa yupo Dodoma.
“Sitatoka Mahakamani hapa kama wao wana uwezo na wanafanya kazi kwa maelekezo waje wanikamatie hapa mahakamani, sitoki nitaendelea kunywa maji yangu haya yatanipa nguvu ya kukaa hadi jioni,” alisema Lissu.
Aidha Lissu alisema aliamua kubaki mahakamani baada ya kudokezwa kuwa kuna gari linamsubiri nje ya mahakama kupelekwa Dar es Salaam. Katika mazingira ya mahakama kulikuwa na watu walioonekana kusubiri wakiwa katika mavazi ya kiraia huku gari la Polisi likiwa limeegshwa jirani na lango la kuingilia viwanja vya Mahakama hiyo.
0 Comments