Seneta wa Trump apatwa na saratani ya ubongo

Seneta wa Trump apatwa na saratani ya ubongo


Chama cha Republican cha rais Donald Trump kimepata wakati mgumu baada ya seneta wake John McCain kupatikana na saratani ya ubongo.


McCain ambaye pia aliwahi kugombea urais kupitia chama hiko mwaka 2008, alikutwa na uvimbe huo wakati wa upasuaji wa kuondoa damu ilioganda juu ya jicho lake la kushoto.

Upasuaji huo ulifanyiaka siku ya Ijumaa katika hospitali ya Phoenix katika jimbo la Arizona. Kwa mujibu wa madaktari wa kiongozi huyo wamesema kuwa matibabu yake huenda yakashirikisha matumizi ya dawa au mionzi.

Uchunguzi wa kitabibu uliofanyika ulibaini kwamba uvimbe wa ubongo unaojulikana kama Glioblastoma ulisababisha damu hiyo kuganda. Hata hivyo madaktari hao wamesema afya ya McCain inaendelea kuwa nzuri.

Glioblastoma ni uvimbe unaotokea kwenye ubongo na huongezeka kutokana na umri wa mtu na huwakumba zaidi wanaume kuliko wanawake.

Post a Comment

0 Comments