Rose Muhando.
STAA wa nyimbo za Injili, Rose Muhando amefunguka kuwa, haogopi watu wanaomsema kwa ubaya kila kona bali anaangalia kile kilichomsababisha kuwa mwimbaji ambaye nyimbo zake zinawabariki wengi.
Rose aliliambia Wikienda kuwa, watu wamekuwa wakimzushia mambo mengi ya ajabu, lakini hawajui anachokifanya kwa sasa ila siku wakija kugundua wataumbuka ndiyo maana yupo kimya hata kwenye muziki huo hivyo wanaomsema na kumtakia mabaya anawaombea kila kukicha na Mungu atawalipa kila mmoja kwa wakati wake.
“Najua aliyeniita katika huduma ya uimbaji ni Mungu na siyo mwanadamu, hivyo kwa kila jambo namsikiliza yeye siyo mwanadamu mwenzangu, siogopi wanaonisema vibaya maana ninaamini aliyeniita hataniacha,” alisema Rose ambaye mara kwa mara amekuwa akiandikwa kwa stori za utapeli.
0 Comments