Hamisa Mobeto
WAKATI yakisemwa mengi juu ya ujauzito alionao ambao kwa sasa hauhitaji miwani ili kuuona, mwanamitindo matata Bongo, Hamisa Mobeto amepasua jipu juu ya mimba hiyo kufuatia kutajwa kwa msanii wa Bongo Fleva.
Kwa siku kadhaa sasa, kumekuwa na habari nyingi juu ya Hamisa kudaiwa kubeba ujauzito wa jamaa huyo ilihali akijua msanii huyo ana mpenzi wake ambaye amekuwa akikwaruzana naye mara kwa mara.
HAMISA AJIFICHA
Ilielezwa kwamba, kufuatia maneno mengi juu ya jambo hilo, Hamisa amekuwa akijifi cha kukwepa vyombo vya habari, lakini Wikienda limefanikiwa kumbana na kufunguka mazito.
Hamisa Mobeto akionyesha.
KWELI MJAMZITO
Hamisa ambaye wengi wamekuwa hawana uhakika kama kweli ni mjamzito, mbali na kukiri kuwa kweli ni mjamzito wa mtoto wa pili baada ya yule wa awali wa kike aliyezaa na bosi maarufu wa redio jijini Dar, aliliambia Wikienda kuwa, yanasemwa mengi juu ya mimba yake hasa aliyempachika lakini yeye hajali kwani yupo tayari kupokea matusi ya jumla na rejareja.
Wikienda: Je, ni kweli mimba ni ya msanii wa Bongo Fleva kama inavyosemekana?
Hamisa: Siko tayari kusema ujauzito ni wa nani. Watu waelewe hivyohivyo wanavyoelewa.
Wikienda: Lakini kila mtu anajua ni wa msanii huyo, je, ni kweli?
Hamisa: Wanaomtaja baba wa ujauzito wangu hawanisumbui kabisa na wakae wakijua hivyo.
Wikienda: Lakini huoni kwamba ni tatizo kuzaa tena nje ya ndoa baada ya yule wa kwanza uliyezaa na bosi wa redio bila kufunga ndoa?
Hamisa: Hayo ni maisha yangu na kama nilivyosema, maneno ya watu hayanisumbui.
Hata hivyo, mazungumzo kati ya Wikienda na Hamisa yaliishia hapo kwa maelezo kwamba hataki tena kuulizwa jambo hilo kwani kila kitu kinajulikana.
MIMBA YA PILI?
Hii ni mimba ya pili ambayo Hamisa anadaiwa kupachikwa na msanii huyo baada ya ile ya awali aliyopachikwa mwaka jana kuchoropoka na kuwa gumzo kubwa baada ya mpenzi wa mwanaume huyo kuja juu na kuanzisha bifu ambalo halijawahi kuzimwa hadi leo.
0 Comments