NHIF yazindua Bima ya Afya kwa mtoto

NHIF yazindua Bima ya Afya kwa mtoto


Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF) umezindua Bima ya afya kwa watoto (Toto Afya Kadi) yenye lengo la kuwawezesha watoto kupata huduma za afya katika vituo vyote vya afya ndani ya mwaka mmoja.


Huduma hiyo imezinduliwa rasmi leo Jumatatu na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Ummy Mwalimu, katika viwanja vya Mnazi Mmoja.


Akizungumza katika uzinduzi huo Mwalimu amesema lengo ni kutekeleza maelekezo ya serikali yanayotaka watanzania kuwezeshwa kupata huduma za afya kwa urahisi na gharama nafuu.


"Wazazi tuendelee kutoa ushirikiano kuhakikisha kuwa watoto wanapata Toto Afya Kadi ambayo itawawezesha kuwa na uhakika wa matibabu," amesisitiza.


Akizungumza baada ya kopekea kadi, mtoto Khalfan Athumani amesema amefurahi kuwa mmoja wa watoto walisajiliwa katika huduma hiyo.


"Sitopanga tena foleni ninapokwenda hospitali, nawashukuru wazazi wangu na naomba wazazi kote nchini waendelee kuwalipia watoto wao ili kupata huduma ya afya kwa urahisi," amesema.


















Post a Comment

0 Comments