Nimepania sana kwenda Tanzania – Wayne Rooney

Nimepania sana kwenda Tanzania – Wayne Rooney


Baada ya kutangazwa rasmi kujiunga na timu yake ya utotoni ya Everton akitokea Manchester United, Mshambuliaji wa timu ya taifa ya England, Wayne Rooney amefunguka kwa mara ya kwanza kwa kuzungumzia safari ya Everton nchini Tanzania kwa kusema amepania sana kuja nchini.


Kupitia Mtandao wa Klabu ya Everton mapema leo akiwa mazoezini, Rooney amesema hajawahi kufika Tanzania kwa hiyo safari ya Klabu ya Everton kwake itakuwa ni fursa nzuri ya kuifahamu Tanzania ikiwa ni pamoja na kujuana na kutambuana vizuri na wachezaji wenzake.

“Sijawahi kufika Tanzania, na safari hii nimeipania sana kwani itakuwa ni muda mzuri wa kujuana na wachezaji wenzangu, najaribu kuwaza jinsi mechi za ugenini zinavyokuwa na hamasa hususani kwa mashabiki“,amesema Wayne Rooney .

Wayne Rooney ambaye tayari ameshakutana na wachezaji wengine wa Everton kama Michael Keane, Phil Jagielka, Leighton Baines na Ross Barkley wakiwa kwenye Timu ya Taifa ya England.

Post a Comment

0 Comments