Prezzo achimba mkwara Colonel Mustafa

Prezzo achimba mkwara Colonel Mustafa


Rapper Prezzo kutoka Kenya ameamua kukunjua makucha yake kwa msanii mwenzake Colonel Mustafa ambaye amekuwa akimsema vibaya kila kukicha.


Prezzo amedai kuwa Mustafa amekuwa akitoa nyimbo mbovu ambazo hazifanyi vizuri ndio maana amekuwa akitumia jina lake vibaya.

“Huyu jamaa ana ushamba na akili fupi, mimi sijaingia hapa kwa vita au vipi. Jamaa naelewa masahibu yake, anajaribu kutoa muziki leo, hausikiki wala haueleweki na badala akutane na mfalme kama mimi aniambie President mimi carrier yangu ipo mahututi nisaidie na mimi nipate kupenya,” Prezzo amemuambia mtangazaji wa kipindi cha Msetoea cha Citizen Radio, Mzazi Willy Tuva.

Wewe kama utataka kusaidiwa sio utafute bifu na mimi ndio utajwe na kujulikana. Kwa umri niliokuwa nao sasa hivi natosa ngma zilizoenda shuleni, siyo Singida Dodoma. Akijifunza adabu endapo nitampiga busti. Mtu kama Mustafa siyo nitashikana naye mashati, nitavua tu mkanda nimfunde, nimfunde proper halafu akishashika adabu nimsaidie,” ameongeza.

Post a Comment

0 Comments