Tutashughulika na wanaotoa matamshi ya kichochezi – Waziri Mkuu

Tutashughulika na wanaotoa matamshi ya kichochezi – Waziri Mkuu


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amewaonya wanaotoa matamshi ya kichochezi nchini na kusema kuwa serikali itawashughulikia bila ya kujali nyadhifa zao.


Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo Jumatano hii wakati wa ibada ya mazishi ya mke wa Dkt. Harrison Mwakyembe, Linah Mwakyembe yaliyofanyika Kyela jijini Mbeya.

“Tutashughulika na watu wote wanaotoa matamshi ya kichochezi, popote walipo bila ya kujali uwezo wao, vyeo vyao na mamlaka walizonazo,” alisema Waziri Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu amewaomba wananchi wote washirikiane kwa pamoja kumuombea Dkt Mwakyembe na familia yake ili Mwenyezi Mungu aweze kuwafariji.

Na Emmy Mwaipopo

Post a Comment

0 Comments