Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa amekabidhi pikipiki 49 kwa vijana wa wilaya ya Ruangwa ili waweze kujikwamua kiuchumi huku akisema ukiendesha Pikipiki lazima uhakikishe una leseni,bima una kofia ngumu.
Waziri Majaliwa amekabidhi pikipiki hizo Jumatano hii,baada ya kumaliza kuhutubia wananchi kwenye uwanja wa shule ya msingi Likangara.
Baada ya kukabidhi pikipiki hizo, Waziri Mkuu amewataka vijana hao kuhakikisha wanakuwa waaminifu kwa kufanya kazi kwa bidii ili pikipiki hizo ziwe na tija.
“Ukiendesha pikipiki lazima uhakikishe kwamba una leseni, bima, vaa kofia ngumu wewe na abiria wako na marufuku kubeba abiria zaidi ya mmoja.”
Wakizungumza baada ya kukabidhiwa pikipiki hizo vijana hao ambao walikuwa wakiendesha pikipiki za watu ambazo hazina tija, wameahidi kufanya kazi kwa bidii.
0 Comments