Ally Mohammed ’Z-Anto’.
BAADA ya kubamba na Ngoma ya Malavidavi kisha Ukipendwa Ringa, staa wa Bongo Fleva, Ally Mohammed ’Z-Anto’ huenda akafanya kolabo na pacha anayeunda Kundi la P-Square, Peter Okoye.
Peter Okoye.
Akichonga machache na Over Ze Weekend, Z-Anto anayeendelea kutikisa kwa sasa na Ngoma ya Kacheze Unapochezaga alianza kuupongeza uongozi wake wa South For Life (SFL) kwa kumrudisha kwenye gemu na kuhakikisha anaendelea kukua kimataifa kwa kumuunganisha na wasanii wakubwa akiwemo Peter Okoye.
“Ni furaha ya juu niliyonayo. Yote kwa sasa nawaachia South For Life kwani nipo chini yao, endapo mipango itakaa poa basi mtanisikia nikipaa kimataifa,” alisema Z-Anto ambaye kichupa chake kipya kimepikwa na Travellah wa Kwetu Studios.
0 Comments