Bomba la mafuta kupita mikoa minane,vijiji 184

Bomba la mafuta kupita mikoa minane,vijiji 184


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kaleman amesema mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Bandari ya Tanga, utapita katika mikoa minane, vijiji 184 hapa nchini.


Amesema vijiji hivyo vinapatikana katika wilaya 24 zilizopo katika mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga. Bomba hilo litakalogharimu Sh8 trilioni, litakuwa na urefu wa kilomita 1,450.


"Katika vijiji hivyo mradi utapita na wanakijiji watapitiwa na fursa za mradi, ajira 10,000 wakati wa ujenzi zitapatikana na itasaidia kupunguza umasikini,pia kuna megwati 35 zitapatikana kupitia mradi huu,"alisema.


Kauli hiyo ameitoa leo Jumamosi wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima Uganda mpaka Chongoleani Tanga.


Wakuu wa mataifa, Yoweri Museveni na mwenyeji wake, Rais John Magufuli na Serikali wanaongoza sherehe hizo wakiwa wameambatana na na mawaziri, wabunge huku wananchi wakiwa wamejitokeza kwa wingi kufuatilia shughuli hiyo

Post a Comment

0 Comments