Golikipa tegemezi wa Simba kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja

Golikipa tegemezi wa Simba kuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja

Klabu ya soka ya Simba inawajulisha wanachama na mashabiki wake kuwa, Golikipa wake wa kimataifa, Said Mohamed Nduda amepata matatizo ya goti ambayo yamempelekea kupelekwa India kwaajili ya matibabu.


Nduda ambaye aliibuka golikipa bora wa michuano ya COSAFA aliumia mazoezini wakati timu hiyo ikijiandaa kuelekea mchezo wao dhidi ya Yanga SC wiki iliyopita. Matibabu hayo yatamuweka mchezaji huyo nnje kati ya wiki nne hadi sita kabla ya kujiunga tena na wenzake kwaajili ya mazoezi na anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa wiki hii.

Klabu hiyo pia inayo furaha kuwaambia kuwa wachezaji wake, John Bocco na Haruna Niyonzima ambaye alipata majeraha madogo juzi wameshaanza mazoezi na wenzao.

Wakata mchezaji, Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi wa muda mrefu naye anatarajiwa kuanza mazoezi siku chache baada ya madaktari kuthibitisha uzima wa afya yake.

Simba SC inawaomba mashabiki wake kote nchini kuendelea kuiunga mkono timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri kwenye ligi kuu iliyoanza wikiendi iliyopita.

Post a Comment

0 Comments