Jeshi la polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam limetoa taarifa ya uchunguzi wa tukio la kuvamiwa katika ofisi za kampuni ya Mwakili ya IMMMA na kubainisha kuwa watuhumiwa hao walivaa sare za askari.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Benedicto Kitalika alisema watu hao walifika katika ofisi hizo na kuweka mlipuko.
“Majira ya saa 7 na saa 8 usiku watu wasio julikana utambulisho wao na idadi kamili walifika katika ofisi ya Mawakili wa kampuni ya IMMMA advocates wakiwa na madai mawili wakijifanya ni askari kisha kuwachukua walinzi wa jengo hilo na kuondoka nao kwenye moja ya gari waliloondoka nalo ambapo baadae walikutwa eneo la Kawe wakiwa hawajitambui kundi lililobaki liliingia ndani ya ofisi hizo na kuweka milipuko iliyowekwa kienyeji ambapo baada ya watu hao kuondoka ililipuka na kusababisha uharibifu wa mali, majengo ya ofisi hiyo pamoja na majengo ya jirani,” alisema Kamanda Benedicto.
“Jeshi la polisi kanda Maalum linapenda kuwahakikishia wananchi kuwa linaendelea kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini watu hao waliofanya tukio hilo pamoja dhamira yao ili wakamatwe na kufukishwa mbele ya sheria.”
Tukio hilo la kuvamia ofisi za IMMMA lilitokea Agosti 26 mwaka huu.
0 Comments