Wanafanya muziki kwa ushindani – Alikiba

Wanafanya muziki kwa ushindani – Alikiba


Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka kwa mara ya kwanza kwa kusema kuwa kuingiliana ratiba kwenye kutoa ngoma kwenye muziki wetu ni kitu cha kawaida kwani wasanii wengi wanafanya muziki kwa kushindana.

Alikiba

Alikiba amesema kinachosababisha wasanii kuingiliana kwenye ratiba za kuingiliana kwenye ratiba ya kutoa nyimbo ni kutokana na kukosa umoja kwenye muziki wetu ingawaje yeye huwa haangalii msanii mwingine kafanya nini ili yeye atoe ngoma kushindana nae.

“Mimi kwa jinsi ninavyoona, naona kama ni sawa tu ni kwa sababu kukosekana kwa umoja unajua hata wenzetu (Wasanii wa nje) wanashauriana ili wasaidiane kusapoti na kuachiana nafasi ila kwa mimi sijaona kama kuna chochote kwa sababu umoja hakuna, hakuna umoja na watu wanafanya muziki kama ushindani, mimi huwa sifanyi hivyo…naachia ngoma zangu kwa ratiba sikufikiria mtu atoe nyimbo na mimi ndiyo nitoe ngoma,”amejibu Alikiba swali aliloulizwa kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio jana lililohoji kuhusu kuingiliana kwenye ratiba za utoaji wa nyimbo.


Mjadala mkubwa kwa sasa nchini Tanzania kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva ni kuhusu muingiliano wa nyimbo mbili za wasanii wakubwa nchini Alikiba wimbo wake wa ‘Seduce Me’ na wimbo wa ‘Zilipendwa’ wa WCB ambapo nyimbo hizo zimepishana masaa 12 kutoka huku wengi wakihusisha kitendo hicho kama cha ushindani baina yao.

Post a Comment

0 Comments