Madaktari wasimamisha upasuaji wa mama mjamzito wakitaka kupigana (+video)

Madaktari wasimamisha upasuaji wa mama mjamzito wakitaka kupigana (+video)


Madaktari wawili nchini India wameishia chupuchupu kurushiana makonde kwenye chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Umaid walipokuwa wakimfanyia upasuaji mama mjamzito.

Video na picha za tukio hilo zimesambaa kwenye mitandaoni ya kijamii zikiwaonesha Madaktari hao wakiacha majukumu yao huku wakizozana.

Taarifa rasmi kutoka kwa viongozi wa Hospitali hiyo iliyopo mjini Rajastham imethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku wakisema tayari madaktari hao wamesimamishwa kazi kwa muda, ingawaje haijajulikana chanzo cha kuvuja kwa picha hizo.

Mara baada ya kuvuja kwa mkanda huo wa video mtandaoni, ripoti nyingi zilidai kuwa mwanamke anayeonekana akiwa katika meza ya upasuaji alizaa mtoto ambaye baadae alifariki.

Hata hivyo, Dkt Ranjana Desai, mkuu wa Hospitali ya Umaid amekanusha madai hayo kwa kusema kuwa mtoto na mama yake wako salama.

”Wakati nilipoina video hiyo, na kufanya uchunguzi wa ndani kwa ndani, vyombo vya habari tayari vilikuwa vimetangaza kuwa, mtoto huyu alikuwa amefariki, ukweli ni kwamba mama na mtoto wapo salamaKuna mtoto amefariki lakini siye ambaye vyombo vya habari vilitangaza,”amesema Dkt Desai kwenye mahojiano yake na BBC.

Kwenye Video, ambayo imesambazwa mitandaoni madaktari hao wanasikika wakirushiana matusi mazito mazito kwa lugha ya Kihindi, na kuanza baadaye kugombana huku mgonjwa akiwa amelala kwa ajili ya upasuaji.

Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt Desai tayari amewatambua madaktari hao wawili na kutaja majina yao kuwa ni Dkt Ashok Nanival na Dkt Mathura Lal Tak huku akisema Madaktari hao hawajafutwa kazi bali wamesimamishwa kazi kwa muda ili kupisha mamlaka kuu ya Hospitali hiyo kuendelea na uchunguzi dhidi ya kisa hicho.

Mahakama kuu ya jimbo la Rajasthan imeamuru Hospitali hiyo kutoa ripoti ya kina, huku mahakama hiyo ikitekeleza uchunguzi wao kuhusiana na kisa hicho.

Tazama video ya tukio hilo

Post a Comment

0 Comments