Tangu tukiwa wadogo tulikua tukiambiwa kwamba dawa huharibiwa na maziwa iwapo zikitumika pamoja.
Mimi binafsi nilipata tabu kidogo kwani baba yangu alikua daktari na alikua akinipa dawa na maziwa na hata nilikua nikimuuliza kuhusu madai ya watu mtaani alikua hanipi jibu.
lakini baada ya kwenda chuo cha udakaktari kuna mambo ambayo nimejifunza na kuelewa kuhusu swala hili la maziwa na dawa.
Je dawa zote zinamalizwa nguvu na maziwa?
Jibu la hapa ni ndio na hapana, kiukweli ni kwamba ni dawa chache sana ambazo zinaingiliana na matumizi ya maziwa na dawa nyingi sana hazina shida na maziwa.
Maziwa yana madini ya calcium ambayo ndio yanafanya baadhi ya dawa zikatae kwenda na unywaji wa maziwa.
Mfano dawa za magnesium ambazo hutumika mara nyingi na watu ambao wana madonda ya tumbo au ambao wanasikia matumbo yao yamejaa gesi haitakiwi kutumika na maziwa kwani madini ya magnesium na calcium hupambana ili kumeng'enywa na mwili hivyo ukinywa maziwa dawa haitafanya kazi vizuri.
Mfano mwingine ni dawa za jamii ya tetracyline kama doxycyline ambayo ikitumika na maziwa haifanyi kazi vizuri yaani hupungua nguvu, lakini dawa nyingi zilizobaki huwa hazina shida.
Je kuna faida ya kunywa maziwa na dawa?
Baadhi ya dawa zinafanya kazi vizuri zikimezwa na maziwa, mfano hai ni dawa ya mseto ya malaria ambayo ili ifanye kazi vizuri inatakiwa iambatane na vyakula vya mafuta kama maziwa, nyama au maparachichi hivyo kutumia dawa hii na maziwa ni bora zaidi kuliko kumeza na maji.
Dawa zingine za maumivu kama diclofenac, diclopa, ibuprofen, meloxicam, peroxicam [ambazo zipo kwenye kundi la non steroidal ant inflamatory drugs], ni nzuri zaidi zikitumika na maziwa kuliko maji kwani zina tabia ya kuchubua utumbo na kusababisha madonda ya tumbo.
Nini cha kufanya?
Ni vizuri ukawa makini wakati unapewa dawa hospitaini ili kufuata maelekezo, kama wewe ni muoga wa dawa chungu unaweza kuinywa na soda, juice au hata maziwa.
tusikariri tu kwamba kila dawa inamalizwa nguvu na maziwa...mimi binafsi sijawahi kunywa dawa kwa maji tangu nimezaliwa.
0 Comments