Mkuu wa wilaya awasamehe waliopopoa mawe msafara wake

Mkuu wa wilaya awasamehe waliopopoa mawe msafara wake



Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Simon Odunga, amewasamehe wanakijiji wa Mlongia kata ya Jongolo waliobeba silaha za
kijadi, virungu na mawe wakidaiwa kuupiga mawe msafara wa Kamati ya
Ulinzi na Usalama wa wilaya hiyo ulipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi
katika kijiji hicho.
Akizungumza jana Jumatatu, Odunga amesema ameamua kuwasamehe na kutowafikisha mahakamani wakazi hao wanaodaiwa kuhusika katika vurugu hizo baada ya makubaliano kuwa hawatarudia tena kitendo kama hicho.
“Haina haja ya kuendelea na ugomvi na wananchi ambao unawaongoza.
Niliwasamehe na waliapa kutorudia tena vitendo kama hivyo na sasa hali
imetulia,” amesema Odunga.
Tukio hilo lilitokea Januari mwaka huu wakati Kamati ya Ulinzi na
Usalama ya Wilaya hiyo ilipokuwa ikenda katika mkutano huo uliolenga
kujadili mgogoro wa ardhi kati ya wakazi wa kijiji hicho na mwekezaji
aliyetambulika kwa jina la Msukuma, ambaye anadaiwa kupewa ekari 500
kwa ajili ya kuwekeza katika eneo la kijiji hicho.
Kwa mujibu wa Odunga, hakuna haki ambayo imekiukwa na mwekezaji
huyo bali mvutano huo ulitengenezwa na wanasiasa.
“Hakuna haki ya msingi ambayo imekiukwa katika eneo hilo isipokuwa
mgogoro huo umesababishwa na elimu ndogo na wanasiasa kuwachochea
wananchi,” alisema.
Alisema kimsingi shamba hilo la mwekezaji lenye ukubwa wa ekari 450 liko katika kijiji cha Kwadelo wilaya ya Kondoa na wala si wilaya ya Chemba.
“Na viongozi wa Wilaya ya Kondoa wanamtambua mwekezaji huyo lakini
wanasiasa hawa wamekuwa wakimpiga vita tangu mwaka 2006, sijui ni
kwa sababu gani,” alisema.
Katika tukio hilo, wanakijiji hao wakiwa na silaha za jadi, mapanga,
virungu na mishale walishambulia Kamati ya Ulinzi na Usalama na
kuharibu pia gari ya Mkuu wa Usalama wa Wilaya baada ya kulipiga mawe.
Tukio hilo lilisababisha watu 30 kukamatwa akiwemo mwenyekiti wa
kijiji na kuhojiwa kuhusiana na fujo hizo.a



Post a Comment

0 Comments