Trump amfukuza kazi mwingine

Trump amfukuza kazi mwingine


Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ya White House, Anthony Scaramucci, amefukuzwa kazi siku 10 tu baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Scaramucci, ambaye amefanya kazi kwa kipindi kirefu Wall Street, amekosolewa baada ya kumpigia simu mwaandishi mmoja na kuwasema wafanyakazi wenzake wa Ikulu.
Mkuu wa utumishi wa umma wa Trump, Reince Priebus na msemaji wake, Sean Spicer wote walijiuzulu kutokana na uteuzi wa Scaramucci siku kumi zilizopita.
Uamuzi wa kumfukuza kazi umefanywa na mkuu mpya wa utumishi wa umma wa Trump, John Kelly, ambaye aliapishwa Jumatatu.
Taarifa fupi kutoka White House imesema: "Anthony Scaramucci atauacha wadhifa wake kama Mkurugenzi wa Mawasiliano wa White House.”
Awali, Trump alikuwa ameandika kwenye Twitter kuhusu takwimu za nafasi za kazi na ajira na akasisitiza kwamba hakukuwa na mgogoro wowote White House.
Awali, Scaramucci alikuwa ameringa kwamba huwa anaripoti moja kwa moja kwa Rais Trump badala ya kupitia kwa mkuu wa utumishi wa umma.
Reince Priebus alijiuzulu Ijumaa baada ya Scaramucci kuandika ujumbe kwenye Twitter na kisha kuufuta, ambapo wengi waliufasiri kama tuhuma na tishio dhidi ya Priebus.

Post a Comment

0 Comments