Msanii wa muziki wa Pop na RnB kutoka Marekani, Neyo amemjumuisha Msanii kutoka Tanzania Diamond Platnumz kwenye ziara yake ya kimuziki nchini Uingereza.
Orodha ya miji na kumbi atakazotumbuiza Ne-Yo na Diamond Platnumz kwenye ziara yake nchini Uingereza
Ne-Yo amethibitisha hilo na kutoa ratiba yake kamili ya Tour yake ambayo iliahirishwa mara mbili, mwishoni mwa mwaka jana na mwezi Machi mwaka huu baada ya kutokea mashambulizi ya kigaidi jijini Manchester nchini Uingereza.
Tour hiyo itaanza tarehe 13 hadi 23 Septemba mwaka huu na atatumbuiza miji nane nchini humo kote akiwa na Diamond Platnumz.
Hii inakuwa ni ziara kubwa ya kwanza kwa Diamond Platnumz kupewa shavu la kutumbuiza kwenye tour ya Msanii mkubwa duniani, hivyo watanzania tusubiri neema kwenye muziki wetu itakayopatikana baada ya ziara hiyo iliyopokelewa kwa mikono miwili na Waingereza.
0 Comments