MUIGIZAJI nyota wa filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ mwishoni mwa wiki iliyopita aligeuka kuwa gumzo baada ya nguo aliyovaa kuonekana kumtesa kutokana na matiti yake kutaka kuchomoza kila wakati.Tukio hilo lilitokea katika Ukumbi wa Cinema, Mlimani City Jumamosi iliyopita wakati wa uzinduzi wa Filamu ya Heaven Sent ya muigizaji mwenzake, Wema Sepetu ambayo ilikutanisha mastaa wa fani mbalimbali nchini.
Lulu aliyekuwa amependeza kwa mavazi yake, akiwa amevalia gauni jeusi refu lenye mpasuo mkubwa, alijikuta akipata taabu ya kuirudisha nguo yake sehemu ya kifuani, kwani kila wakati matiti yalionekana kutaka kutoka nje, lakini akawa anafanya kazi kubwa ya kuirudishia.
Jamani muoneni Lulu anavyohangaika na hiyo nguo, sasa tangu nyumbani hakujua kama inamsumbua abadilishe? Au ndiyo mbwembwe za kutaka watu waone nido zake zilivyo nzuri?” alisikika akisema shabiki mmoja aliyeonekana kumfuatilia sana muigizaji huyo.
Licha ya Lulu, mastaa wengine kibao wa filamu walihudhuria uzinduzi huo na mashabiki wa kawaida wa tasnia hiyo, huku Wema Sepetu mwenyewe akiwa amesindikizwa na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani, mshindi wa Big Brother Hotshot, Idris Sultan. STORI: RICHARD BUKOS
0 Comments