Nyama ya Punda yazidi kupanda bei, watumiaji walalamika

Nyama ya Punda yazidi kupanda bei, watumiaji walalamika



Shirika moja la kutetea wanyama nchini Kenya limesema bei ya Punda imepanda maradufu nchini humo kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya nyama ya mnyama huyo nchini China taifa ambalo hununua kwa wingi bidhaa ya mnyama huyo.


Kwa mujibu wa shirika hilo, sababu ya bei ya Punda kupanda kwa karibu 200% ni kutokana na ongezeka la biashara ya bidhaa za mnyama huyo huko Uchina ambako nyama ya punda ni kitoweo kilicho na walaji wengi.


Mataifa kadhaa ya Afrika yamepiga marufuku uuzaji wa nyama na bidhaa nyinginezo za punda, nchini China kwa sababu mnyama huyo ambae hutumiwa zaidi kwa ajili ya kusaidia kubeba mizigo mashambani, sasa idadi yao inapungua kwa kasi mno.


Baadhi ya Mataifa ya Afrika yaliyopiga marufuku uchinjaji na uuzaji wa nyama ya Punda ni pamoja na Uganda, Tanzania, Botswana, Niger, Burkina Faso, Mali, na Senegal.

Post a Comment

0 Comments