Majanga yameendelea kuikumba klabu ya Arsenal ambapo safari hii watu wanaosadikiwa kwamba ni vibaka wamevamia duka la klabu hiyo lililopo uwanja wao wa nyumbani wa Emirates na kuiba.
Vibaka hao walivunja baadhi ya vitu ikiwemo bendera kubwa ya klabu hiyo iliyopo nje ya duka hilo na kisha kuzama ndani na kuiba baadhi ya bidhaa ambazo zilikuwemo ndani ya duka hilo usiku wa Jumanne.
Baada ya tukio hilo wezi hao walitoka njr na kupakia gari kisha kukimbia na kuwaacha watu walioko eneo na jirani hilo kushikwa na butwaa,muda mfupi baada ya tukio hilo polisi wa kitongoji hicho cha Islington walifika uwanjani hapo.
Polisi hao wamewataka raia wa karibu na eno hilo kutoa taarifa za kuwezesha kuwakamata waliofanya tukio hilo la kihalifu kupiga simu maalumu namba 101 kutoa taarifa.
Tukio hilo la wizi linakuja siku chache baada ya klabu hiyo kupokea kipigo cha mabao 4 kwa sifuri kutoka kwa Liverpool kipigo ambacho kiliibua hasira za mashabiki wa Arsenal lakini kipigo hicho bado hakijahusishwa na tukio hili.
0 Comments