Watoto waliodaiwa kutekwa, wawili wapatikana

Watoto waliodaiwa kutekwa, wawili wapatikana



IKIWA ni siku chache baada ya vyombo vya habari kuripoti kuhusu kupotea kwa watoto wanne waliodaiwa kutekwa, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amethibitisha kupatikana kwa watoto wawili na kumshikilia mtu mmoja aliyekutwa na watoto hao katika Kata ya Olasiti .

Kamanda Mkumbo amesema jeshi lake linaendelea na upelelezi kuhakikisha watekaji wote wanapatikana kwani tukio hilo sio la kufumbia macho na pia lina hatarisha amani kwa wakazi waJjiji la Arusha.

Wazazi watoto waliopatikana wameeleza kuwa watoto wao waliletwa na dereva wa boda boda mara baada ya watekaji kupatiwa namba ya balozi na kuwaagiza kuwarudisha nyumbani watoto Ayub Fred na Bakari Suleman.

Mama mzazi wa Bakari amesema ni faraja kuona mwanae amerudi salama nyumbani mara baada ya kumpoteza kwa siku nne mara baada ya kutekwa na watu wasio fahamika.

Amesema wazazi wengine wasikate tama kwani jeshi la polisi bado linaendelea na msako wa kuwapata watoto wengine wawili Maurin David pamoja na Ikram Salim ambapo mpaka sasa hawajulikani walipo.

Awali watekaji hao waliripotiwa kuwapigia simu wazazi wa watoto hao ili wawapatie pesa ndipo wawarudishe watoto hao majumbani mwao.

Post a Comment

0 Comments